Sunday, 19 July 2020

Ufalme wa mbinguni unaanzia duniani......


Habari za wakati huu rafiki yangu, tuna kila sababu ya kumshukuru mungu kwa afya na uzima kwa wiki nzima na changamoto tulizopitia ni sehemu ya kutuimalisha kwani hakuna jaribu utakalopitia likakuacha dhaifu,kama halijakuua Basi limekuimarisha ki roho au ki akili......

Leo tupate neno kutoka kwa Mwinjili Mathayo (Mt:13:24-43)
Kupitia mwinjili Mathayo kwenye somo tajwa hapo juu tunaweza kuona yesu akiongea na makutano kwa kutumia mifano,kabla hatujaangalia mifano hiyo utakubaliana na Mimi kwamba maisha ya mbinguni ambayo Mimi na wewe tunayatamani kuishi baada ya kukamilisha maisha ya duniani, ikiwa mungu mwenyewe kupitia mwanae yesu kristo aliyaishi maisha ya dunia na mwisho akayashinda mauti basi na sisi lazima tujiulize na kufahamu msingi utakao tufanya siku moja tuyaishi maisha hayo ya umilele.

Kupitia masomo hayo yesu alitumia mifano mitatu akiifananisha na namna ufalme wa mbinguni unavyofanana, kupitia mifano hiyo tutaangalia mifano miwili tukiifananisha na maisha yetu ya Kila siku.

*1.Mfano wa ngano*
Kwenye mfano wa ngano na magugu tunapata funzo kubwa sana, wakati ukipanga mambo yako kwa usahihi kabisa na mipango mizuri kama tulivyoona kwenye mfano wa Shamba la ngano, mbegu bora na Shamba safi kabisa basi kitu tunachotarajia ni kupata mavuno safi yasiyo na changamoto yoyote, lakini baada ya muda kupita na ngano inapoanza kutoka inaambatana na magugu, magugu ni mfano wa changamoto ambazo zinaibuka pamoja na mipango mizuri tuliyoipanga, pamoja na changamoto hizo je maamuzi ni yapi? Kupitia neno la mungu tunafundishwa kwamba pale tunapopitia changamoto basi tunapaswa kuvumilia kwani kupitia somo nililokushirikisha tunaona watumwa wakishauri magugu kung'olewa lakini yesu anawajibu tusifanye hivyo tuyaache yakuwe pamoja na ngano na wakati wa kuvuna ndipo tutachambuwa ngano na kufunga matita magugu na kuyachoma moto, hapa tunapata funzo la kwamba safari ya maisha, safari ya mbinguni ni safari ambazo huwezi kujitenga na changamoto, kupoteza watu tunao wapenda, kujaribu biashara na kushindwa ni magugu kwetu, lakini hayo yote yanavyojitokeza kwanza tunapaswa kuyakubali na kuona ni sehemu ya ubinadamu wetu lakini mwisho utafika na mungu atatutenganisha na magugu, shida na mateso, hapa ndipo tunaona kwamba uvumilivu ni njia ya kweli ya kutufanya tushinde duniani na mbinguni.

*2.Mfano wa punje ya haradani*
Inasemekana haradani ndio mbegu ndogo kuliko zote, wakati nasoma hapa nikajiuliza kama punje ya ulezi ni kubwa kwa punje ya haradani Je hiyo punje ya haradani inafananaje? Lakini biblia inatuambia pamoja na udogo wa punje hii lakini ikiota inakuwa kubwa kuliko mboga zote na kutengeneza matawi ambayo hata nyuni wa angani hutua katika matawi yake. Rafiki haijalishi udogo wako ulio nao sasa, ki uchumi,ki mamlaka, ki umri na ki mtazamo lakini ukijifananisha na mbegu ya haradani unapata tumaini ya kwamba unaweza kuwa vyovyote unavyotaka.

Nini nimejifunza kwa somo hili?
Ushindi huja mwishoni baada ya maangaiko namateso ya muda mrefu wa kuvumilia na kujitoa kutafuta unachotaka bila kuchoka, safari ya yesu kwetu wakristo ni ki elelezo tosha, alibezwa, aliteswa,alitemewa mate na mengine mengi lakini alivumilia yote kwasababu alifahamu nini alikitafuta na mwishoni tunaona anaibuka Mshindi zidi ya mauti na kutukomboa, Je wewe unataka nini? Ufalme wa mbinguni, maisha ya utajiri na kusaidia wahitaji? Upo tayari kukabiliana na mateso yapi? Kipi unavumilia ili ushinde mwisho? Ukisemwa na kukosolewa unakasilika au unafahamu ni njia ya kufika unakotaka kufika? Vipi ukitemewa mate utakubaliana? Utavumilia? Nenda kayaishi haya kwa vitendo na mwishoni tutakutana pamoja tukishelekea ushindi pamoja.

Makala hii imeandikwa na Kelvin Kinyaga, mwalimu na mwanafunzi wa elimu ya fedha kupitia Chuo cha Kisima cha maarifa tutakutana kesho tukifanyika Baraka.

Kinyagakelvin162@gmail.com

https://kinyagakelvin.blogspot.com

0712161251/0763766944

No comments:

Post a Comment