Sunday, 12 July 2020

UTANGULIZI



Karibuni kwenye darasa letu maalumu la Leo tarehe 12/07/2020,Kwenye darasa hili tutajifunza jinsi ya kupakua App yenye uwezo wa kutunza taarifa zako zote za fedha na namna ya kuitumia application hiyo.

Kwanza kabisa app hii alitushirikisha kocha terehe 03/02/2020 na kwa kuona ni kitu muhimu nilichukuwa ujumbe huo na kuuhifadhi kwenye stared messages na sikuhangaika nao kwa siku hiyo, huwa na kawaida wa kupitia message zilizohifadhiwa baada ya muda fulani kupita, kwenye mwezi wa tano mwishoni nilianza kufanyia kazi application hii na mpaka sasa nimeona faida zake na kwenye maswali mengi ya taarifa yangu ya mwezi sipati shida kuandaa kwani naweza zichukuwa taarifa zangu kutoka kwenye App hii na kuwasilisha kwenye taarifa yangu, hapa chini ni ujumbe huo Kila mmoja aupitie upya kama ulishaupoteza, karibuni tujifunze pamoja Nina imani kuna kitu mtaondoka nacho na mwishoni mtaweza kuongezea na kuuliza maswali ili kupata ufafanuzi zaidi, unaweza kujifunza kwa vitendo kwa kufanya kile ninachokuelekeza, karibu sana rafiki yangu.

Huu hapa chini ujumbe wa kocha wa tarehe 03/02/2020.

Hii apa chini nayo ni Mobile App inaitwa  inaitwa  Vmoney tracker-Money manager and budget planner.

Nayo ni nzuri sana katika utunzaji wa taarifa zako zote  kifedha kwa kadri zinavyoingia na zinavyotoka. Hii App is the best sababu imesheheni vitu vingi sana sana na unaweza kuingiza data zako mpka ikakupa balance sheet yako ya fedha.Ina categories nyingi sana na inakupa uwanja mpana wa kutunza hesabu zako kifedha.
Faida kubwa ni ile ile tu kwamba unaweza kurekodi taarifa zako muda wowote wakati wowote pale unapoingiza au kutoa fedha.



https://play.google.com/store/apps/details?id=com.voutputs.vmoneytracker

No comments:

Post a Comment