Wednesday, 24 June 2020
Umuhimu wa mifereji mingi na mifereji unayopaswa kuwa nayo...
Rafiki karibu tuendelee kuwa sote na tuweze kujifunza pamoja, lengo ni kuhakikisha mateso yetu na ya wengine yanapunguwa kwani hata mwenyezi mungu anatambuwa kukosa maarifa kunatuangamiza, karibu twende pamoja.........
Siku alhamisi ni siku ambayo tunachambuwa kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA na wiki hii tutaweza kuona umuhimu wa kuwa na vyanzo vingi vya mapato ambavyo vinakuingizia fedha.
Mwandishi anafananisha hali ya kuwa na vyanzo vingi vya mapato kama mito mingi ambayo inatiririsha Maji yake kuelekea bahari moja.Pale mto mmoja ukikauka basi bahari itaendelea kupokea Maji kutoka kwenye mito mingine, hebu chukulia mfano wa tangu umeanza kusikia bahari ulishawahi kusikia bahari imekauka? Basi pale unapokuwa na chanzo cha aina moja cha kukuingizia fedha basi huwezi fikia utajiri na unakuwa kwenye hatari kubwa pindi unapopoteza kazi hiyo.Mwandishi anaweza kutuonyesha utafiti uliofanywa na waandishi wa kitabu cha THE MILLIONAIRE NEXT DOOR na walibaini kwamba baada ya kufuatilia maisha ya matajiri wenye utajiri wa zaidi ya billion 2 za Kitanzania walibaini hakuna tajiri aliyekuwa anategemea kipato cha aina moja, waajiriwa na wafanyabiashara wadogo tuko kwenye changamoto nyingi kwasababu ya kutegemea kipato cha aina moja mwandishi anasema ni hatari kubwa sana hii kwenye fedha na utajiri.
MIFEREJI YA KIPATO UNAYOPASWA KUITUMIA
Vipo vyanzo vingi sana vya mapato unavyoweza kuvitumia lakini mwandishi amevigawa kwenye makundi yafuatayo.
1.Kazi au ajira,hapa unaweza kuwa umeajiriwa au kujiajiri na unauza ujuzi na muda wako ili kupata fedha.Hiki siyo chanzo kizuri kwasababu kitakupa ukomo wa fedha na muda. Lakini ni chanzo ambacho wengi wanaweza kuanzia hapa kuelekea safari ya utajiri.
2.Biashara, hapa unauza bidhaa au huduma kwa watu wengi na kuweza kutengeneza faida.kundi hili unaondoka kwenye ukomo wa muda na wewe binafsi,hapa unakuwa na mfumo ambao utakuwezesha kutumia muda wa wengine,nguvu za wengine na ujuzi wa wengine kuweza kutengeneza kipato.
3.Uwekezaji;Hapa unaiwekeza fedha yako sehemu inayozalisha na kisha unapata faida, hii ndio dhana ya fedha kukufanyia kazi,unapata gawio au riba kulingana na uwekezaji ambao unakuwa unafanya. Mbele utaona makundi yaliyogawanyika kwenye kuwekeza.
4.Mrahaba; Hapa unalipwa kwa kazi ambayo ulishaifanya huko nyuma.Waandishi wa vitabu wanaingia kwenye kundi hili, ukishaandika kitabu kazi yako inakuwa kuchapa na kuongeza nakala zaidi. Hivyo mwandishi anashauri acha kufikiria sehemu moja ya kipato,unaweza kuwa na biashara zaidi ya moja, ukawa na uwekezaji kwenye Mali, ukawekeza kwenye hisa na kununua vipande.
Hili ni zoezi muhimu kulifanya kwa Kila mmoja ingawa litachukuwa muda mrefu kulifikia, hivyo unaanza kidogo kidogo, siyo Leo umeanza biashara moja na haijasimama vizuri unaanza biashara nyingine,lazima kile ulichoanza mwanzo kisimame vizuri ndipo uanze kingine,lakini usikubali kuwa na maisha ya chanzo kimoja cha kipato. Asante rafiki tukutane wiki ijayo kuendelea na chambuzi ya kitabu hiki.
Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment