Saturday, 14 March 2020

Tengeneza changamoto na utatuzi wake kabla hazijatokea......

Rafiki yangu hongera na mapambano unayoendelea nayo hata kama hali ni ngumu kiasi gani lakini wagumu wanadumu na sina shaka na wewe kwani natambuwa uwezo na maarifa unayopata yamekuwa Mwanga kwenye kiza unachokabiliana nacho.

Rafiki kitu kikubwa kinachotutesa ni kupata matokeo ambayo hatukuyatarajia,pengine ulisoma kwa bidii lakini hukufaulu mtihani,umepeleka watoto wako shule nzuri lakini hawakupata matokeo mazuri, umefanya kazi kwa bidii lakini matokeo yamekuwa tofauti na matarajio, haya yote unaweza kuona ni bahati mbaya na hukustahili kuyapitia lakini kuwaza hivyo ni kujidanganya. Ipo njia moja sahihi ya kukabiliana na changamoto hii.

TEGEMEA CHANGAMOTO KABLA HAZIJATOKEA.
Rafiki kama umeajiriwa basi ona changamoto ya kulipwa mshahara usio tosheleza mahitaji, ona manyanyaso unayopata kwa boss wako, ona umeshafukuzwa kazi na huna chanzo kingine cha kipato, kisha kaa chini na ona utazitatuaje changamoto hizo sasa kabla hazijatokea.

Rafiki wakati mzuri sana wa kutatua changamoto zako ni wakati mambo yanakwenda vizuri, Je rafiki ni yapi unahisi yanaweza tokea kama changamoto kubwa kwenye maisha yako? Ona imeshatokea na chukuwa hatua sasa ili likitokea lisikuumize kichwa. Ona miaka kadhaa mbele mshahara unaopokea utakatwa makato na kodi nyingi na utapunguwa na anzisha biashara ya pembeni ili utakapopitia hali ngumu zisiwe sababu ya wewe kuto kuishi. Hayo yote yasiwe sababu ya kutoweka bidii, nidhamu na uadirifu kwenye kazi lakini usiweke matarajio yoyote kwani unachokitegemea na kukitarajia ndio kinakufanya uwe mtumwa.
Haya yote yatawezeana kama una falsafa ya kufuata.Karibu tujifunze falsafa bora ya kutupa utulivu na kufanya maisha yaliyokusudiwa.

Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944.

No comments:

Post a Comment