Sunday, 14 February 2021
Kuna Mengi Nimejifunza Kupitia Barua Hii Ya Kumi
Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kukupongeza kwa namna unavyojitoa kutuelimisha,hakika nimejifunza vitu vingi sana kupitia barua hii ya kumi na baadha ni kama ifuatayo.
*Acha kutoa sababu toa matokeo*
Imekua ni kitu cha kawaida pale tunaposhindwa kutekeleza majukumu yetu kwa wakati kutoa sababu na kutaka watu kutuamini kwa sababu hizo.
Kwanza kabisa nianze kwa kukupa pole kwa kuondokewa na mkwe wako,lakini pamoja na hilo kwangu na kwa unayesoma hapa tungetumia sababu hiyo kutokamilisha majukumu yetu na kuona ni sababu ya msingi,ni kweli ni ya msingi lakini hapo ndio panapotofautisha kati ya washindi na washindwa.
*Ushirikina,dini na sayansi*
Hapa kocha umefanya mapinduzi makubwa sana.Kwanza kabisa umeonyesha kwa mifano ni namna gani dini na ushirikina kwa sehemu zinatulazimisha kuamini vitu bila kuhakikisha usahihi wake wakati sayansi inatupa uhalisia wa jambo kwa kurithbitisha.Hakika tunapaswa kuwa makini sana na dini zetu maana tusipoangalia tunakuwa sawa na washirikina.
*Kila dhambi ni zao la ushirikiano*
Dhambi ni makosa ambayo mtu anafanya tena mara nyingi kwa makusudi kabisa.Sasa kwa hili la covid 19 ni kweli kabisa sehemu kubwa ya lawama ziende kwa serikali lakini kwenye hili hata sisi tuna mchango wetu.
kwanza kabisa ni ushabiki wa mambo yasiyo na tija kwetu na kupuuza ukweli ambao uko wazi,jana kwenye jumuiya daktari wa kcmc katupa elimu kuhusu ugonjwa huu lakini cha kushangaza leo kanisani watu wanarudia makosa yaleyale eti serikari haijatangaza hivyo corona hakuna.Sisi tunaotafuta maarifa sahihi tukawe mfano wa kuigwa.Asanteni wote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment