Monday, 7 June 2021
Kitabu cha leo tarehe 07/06/2021
Habari za wakati huu rafiki yangu. Ni mudaa mrefu umepita sijakuandikia ujumbe
wenye mafunzo lakini sasa nitaandika tathimini fupi kwenye siku yangu.
*Ujumbewa leo*
Wakati unafikiria changamoto ulizonazo tambua na zingine nyingi zipo
njiani hivyo ongeza mwendo wa kuzikabiri.
Rafiki yangu moja ya faida kubwa ambayo nimeipata kwenye kujifunzani kuchagua kuanza siku kwa ushindi, je wewe rafiki yangu unaianzaje siku yako?Je unaanza kwa kuangalia habari?je unaanza kwa kuperuzi mitandao ya kijamii?kama unaanza siku yako kwa mtindo huo nakupa pole sana
Maswali mazuri ya kujiuliza.
1.Ni vitu gani nilivyonavyo vya kumshukuru mungu?viandike kwenye diary yako.
2.Je ni namna ni namna gani unatamani siku yako iwe?malengo ya siku.Hakikisha unaipangilia siku yako. usipofanyahivyo wengine watakutumia kwenye siku hiyo kwa manufaa yao.
3.Panga ni namna gani utaongea na mteja wako, kama umeajiliwa boss wako ndio mteja wako.
4.Ni kitabu gani utakwenda kusoma kwenye siku unayoiendea?
Mimi leo nimeweza kukamilisha yale niliyopanga kwa zaidya asilimia 90.Pamoja na ushindi huo zipo changamoto kadhaa nimezipitia.
1.Wakati unapanga muda wako tambua na wengine wameandaa mipango yao kwa kutegemea wewe?Hivyo jiandae kukabiliana na hilo.
2.Zipo tabia mbaya kama kukasirishwa na watu kwa kutaka wawe kama vile unavyotaka wewe, wafanye vile unavyotaka wewe. Kuwa na mtazamo huu ni kujinyima furaha bilasababu.
Asante sana rafiki yangu
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment