Saturday, 12 June 2021
Kitabu Leo#6
Hongera sana rafiki, haijalishi una malengo makubwa kiasi gani hupaswi kuyaogopa anza kuyatekeleza kidogo kidogo, unajuwa nguvu ya matone ya maji kwenye mwamba au jabari kubwa?matone yanaporudia kwa muda mrefu yanavunja mawe makubwa, vivyo hivyo nenda kaanze leo kukamilisha malengo makubwa yaliyopo mbele yako.
"Kuweka akiba %10 ya kipato chako"
Watu wengi hupenda kuuliza naanzaje biashara?
Kipato changu ni kidogo nitatoa wapi mtaji wa biashara?
Rafiki pengine uko njia panda siku nyingi na huoni mwanga mbele na hujui unajitoaje kwenye changamoto za kifedha ulizonazo, madeni yanaongezeka na changamoto mpya zinazaliwa kila kukicha, leo tutajifunza kosa kubwa ambalo umelifanya na unaendelea kulifanya ambalo matajiri wanaijua siri hiyo na ndio maana wanafanikiwa kwenye fedha.
Umekuwa unalipa kodi, unalipa madeni, unalipa ada za watoto, unalipa bili ya maji, unalipa madeni lakini wewe mwenyewe unajisahau
Haijarishi unalipwa kiasi kidogo kiasi gani usikubali kulipa watu wengine halafu ukasahau kujilipa wewe mwenyewe, katika kila kipato unachotengeneza tenga asilimia kumi au zaidi na iwekeze sehemu ambayo hutaweza kuitoa kirahisi, kisha baadae tumia kiasi hicho kikishakua kadri unavyofikiria wewe kwa kupokea ushauri makini kwa watu wenye uelewa kukiwekeza ili kikuzalishie zaidi.
Hii no tabia ya kitajiri nenda kaanze kuiishi mara moja.
Usiache kujiuliza kkusudi la maisha yako ni nini na lengo lako kubwa hapa duniani ni lipi, kisha pambna usiku na mchana kulifikia lengo na kuishi kusudi hilo
kitabu cha maisha yako leo kitaandikwaje?
kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment