Sunday, 13 June 2021

Kitabu Leo#6

Hongera sana rafiki yangu, karibu katika siku nyingine ya ukurasa wa kujifunza na kujifanyia tathimini ni kwa vipi umeweza kuikamilisha siku yako, haijalishi umepitia yapi fahamu lipo kusudi la wewe kuwa hapa duniani na kazi yako ni kulijua na kuliishi. Leo tutaangalia tabia nyingine ambayo unapaswa kuwa nayo ili kuiendea safari ya utajiri na mafanikio. "Tawala hisia zako" Rafiki kama huwezi kutawala hisia ulizonazo fahamu itakuwa vigumu kwako kufanikiwa.Ukiweza kutawala hisia zako pia utakuwa umejiwekea ulinzi kwenye mafanikio yako. Hisia hasi na chanya zote ni kikwazo kwenye maisha yako. Hisia zikiwa juu uwezo wako wa kufikiri unakuwa chini. Mara nyingi ukiwa na furaha sana au na hasira umekuwa na maamuzi ya hovyo sana, na mara nyingine baada ya maamuzi ulianza kujutia kwamba ilikuwaje ukafanya maamuzi ya namna hiyo. Matajiri hawaruhusu hasira,wivu, chukwu,msisimko,huzuni na Sonoma viwatawale. Matajiri HUFIKIRI, kisha HUTATHIMINI halafu HUCHUKUA HATUA. Ratiba zao zimejaa kiasi kwamba hisia haziwezi kuwatawala. Upande wa pili masikini na wasio fanikiwa HUCHUKUA HATUA, kisha HUFIKIRI na WANAPOKUJA KUJITATHIMINI wanakuja kujutia kwani hatua walizochukua zimewaangusha. Watu wasio fanikiwa wana muda mwingi na wanautumia kwa mambo yasiyo na manufaa na hapo huruhusu hisia itawale akili zao. Rafiki jiwekee utaratibu wa baada ya masaa 24 ya kutafakari jambo kabla hujachukua hatua. Fahamu vichocheo vya kupelekea ukashindwa kutawala hisia zako na viepuke. Hakikisha ratiba yako ya siku imejaa, usikubali kukaa tu muda mwingi na kuupoteza. Asante rafiki na nikutakie jioni njema nenda kafanyie kazi haya uliyojifunza. kinyagakelvin162@gmail.com 0763766944/0712161251

No comments:

Post a Comment