Wednesday, 9 June 2021
Kitabu Leo #3
Hongera sana rafiki kwa siku hii ambayo inaelekea ukingoni, bila shaka umeianza kitajiri na unaimalizia kitajiri. Kama hutoimaliza kitajiri ni ngumu kesho kuianza kitajiri.
Hebu fikiria kama unaimaliza siku yako kwa kuangalia TV mpaka saa sita usiku, he utaweza kesho kuamka masaa mawili kabla ya kujiandaa kwenda kazini au kwenye shughuli zako?Kama ulivyojitengea muda wa kuamka basi tenga na muda kulala kila siku na fuata ratiba hiyo.
Leo nimefanikiwa kuanza siku kitajiri kwa kuamka saa kumi na moja na robo, ingawaji nilipata ukinzani mwili kukubaliana akili kwani nilijihisi uchovu na hiyo hutokana na kosa nililofanya la kuchelewa kulala tofauti na muda wangu nilio jiwekea kila siku
Nimefanikiwa kuanza na sala na tahajudi huku nikipata lita moja ya maji ya vuguvugu kama utaratibu niliojiwekea.Kisha kufikiria ni mteja gani ninayetakiwa kuwasiliana naye siku hiyo na kisha kuandaa mpango wa mawasiliano.
*Kitabuni leo na Tabia za kitajiri cha Dr.Makirita amani-ukurasa wa 124 hadi 133*
_Maisha ya kuwa na kiasi_
Moja ya tofauti kati ya masikini na matajiri ni maisha ya kuwa na kiasi, matajiri hawafanyi vitu kwasababu wana pesa ya kufanya bali hufanya kwasababu ni muhimu. Ila masikini wakiwa na fedha wanatamani wanunue kila kitu, anunue nguo,vyombo na kila kitu hata kama siyo muhimu kwake kwa wakati huo.
Matajiri wanafahamu madaraka makubwa huja na majukumu makubwa hivyo huwa makini sana sana kwenye matumizi ya fedha zao. Masikini wakipata fedha kila mtu atafahamu kutokana na kukosa kiasi kwenye matumizi yao.Masikini hukasirika kwa vitu vidogo na huwa na furaha kubwa kwa vitu vya kawaida.
*Vitu vitatu vya kuvifanya siri kwenye maisha yako*
1.Mahusiano yako ya kifamilia.
2.Hali yako kiafya.
3.Kiwango cha fedha ulichonacho.
Matatizo mengi huanzia kwenye mambo haya yanapokuwa wazi kwa kila mtu.
Namshukuru mungu nimefanikiwa kukamilisha mambo matano niliyojipangia kuyakamilisha kwenye siku yangu na nimefanikiwa kutuma ujumbe kwa moja ya wateja wangu kumshukuru kwa kuwa nasi na kumuomba aendelee kufurahia huduma zetu.
Nashukuru kwa siku hii na usiache kujiuliza swali hili. 'Je kama siku yangu hii ingekuwa kitabu kingesomekaje?'
kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944/0712161251
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment