Sunday 13 June 2021

Kitabu Leo#6

Hongera sana rafiki yangu, karibu katika siku nyingine ya ukurasa wa kujifunza na kujifanyia tathimini ni kwa vipi umeweza kuikamilisha siku yako, haijalishi umepitia yapi fahamu lipo kusudi la wewe kuwa hapa duniani na kazi yako ni kulijua na kuliishi. Leo tutaangalia tabia nyingine ambayo unapaswa kuwa nayo ili kuiendea safari ya utajiri na mafanikio. "Tawala hisia zako" Rafiki kama huwezi kutawala hisia ulizonazo fahamu itakuwa vigumu kwako kufanikiwa.Ukiweza kutawala hisia zako pia utakuwa umejiwekea ulinzi kwenye mafanikio yako. Hisia hasi na chanya zote ni kikwazo kwenye maisha yako. Hisia zikiwa juu uwezo wako wa kufikiri unakuwa chini. Mara nyingi ukiwa na furaha sana au na hasira umekuwa na maamuzi ya hovyo sana, na mara nyingine baada ya maamuzi ulianza kujutia kwamba ilikuwaje ukafanya maamuzi ya namna hiyo. Matajiri hawaruhusu hasira,wivu, chukwu,msisimko,huzuni na Sonoma viwatawale. Matajiri HUFIKIRI, kisha HUTATHIMINI halafu HUCHUKUA HATUA. Ratiba zao zimejaa kiasi kwamba hisia haziwezi kuwatawala. Upande wa pili masikini na wasio fanikiwa HUCHUKUA HATUA, kisha HUFIKIRI na WANAPOKUJA KUJITATHIMINI wanakuja kujutia kwani hatua walizochukua zimewaangusha. Watu wasio fanikiwa wana muda mwingi na wanautumia kwa mambo yasiyo na manufaa na hapo huruhusu hisia itawale akili zao. Rafiki jiwekee utaratibu wa baada ya masaa 24 ya kutafakari jambo kabla hujachukua hatua. Fahamu vichocheo vya kupelekea ukashindwa kutawala hisia zako na viepuke. Hakikisha ratiba yako ya siku imejaa, usikubali kukaa tu muda mwingi na kuupoteza. Asante rafiki na nikutakie jioni njema nenda kafanyie kazi haya uliyojifunza. kinyagakelvin162@gmail.com 0763766944/0712161251

Saturday 12 June 2021

Kitabu Leo#6

Hongera sana rafiki, haijalishi una malengo makubwa kiasi gani hupaswi kuyaogopa anza kuyatekeleza kidogo kidogo, unajuwa nguvu ya matone ya maji kwenye mwamba au jabari kubwa?matone yanaporudia kwa muda mrefu yanavunja mawe makubwa, vivyo hivyo nenda kaanze leo kukamilisha malengo makubwa yaliyopo mbele yako. "Kuweka akiba %10 ya kipato chako" Watu wengi hupenda kuuliza naanzaje biashara? Kipato changu ni kidogo nitatoa wapi mtaji wa biashara? Rafiki pengine uko njia panda siku nyingi na huoni mwanga mbele na hujui unajitoaje kwenye changamoto za kifedha ulizonazo, madeni yanaongezeka na changamoto mpya zinazaliwa kila kukicha, leo tutajifunza kosa kubwa ambalo umelifanya na unaendelea kulifanya ambalo matajiri wanaijua siri hiyo na ndio maana wanafanikiwa kwenye fedha. Umekuwa unalipa kodi, unalipa madeni, unalipa ada za watoto, unalipa bili ya maji, unalipa madeni lakini wewe mwenyewe unajisahau Haijarishi unalipwa kiasi kidogo kiasi gani usikubali kulipa watu wengine halafu ukasahau kujilipa wewe mwenyewe, katika kila kipato unachotengeneza tenga asilimia kumi au zaidi na iwekeze sehemu ambayo hutaweza kuitoa kirahisi, kisha baadae tumia kiasi hicho kikishakua kadri unavyofikiria wewe kwa kupokea ushauri makini kwa watu wenye uelewa kukiwekeza ili kikuzalishie zaidi. Hii no tabia ya kitajiri nenda kaanze kuiishi mara moja. Usiache kujiuliza kkusudi la maisha yako ni nini na lengo lako kubwa hapa duniani ni lipi, kisha pambna usiku na mchana kulifikia lengo na kuishi kusudi hilo kitabu cha maisha yako leo kitaandikwaje? kinyagakelvin162@gmail.com 0763766944/0712161251

Wednesday 9 June 2021

Kitabu Leo #3

Hongera sana rafiki kwa siku hii ambayo inaelekea ukingoni, bila shaka umeianza kitajiri na unaimalizia kitajiri. Kama hutoimaliza kitajiri ni ngumu kesho kuianza kitajiri. Hebu fikiria kama unaimaliza siku yako kwa kuangalia TV mpaka saa sita usiku, he utaweza kesho kuamka masaa mawili kabla ya kujiandaa kwenda kazini au kwenye shughuli zako?Kama ulivyojitengea muda wa kuamka basi tenga na muda kulala kila siku na fuata ratiba hiyo. Leo nimefanikiwa kuanza siku kitajiri kwa kuamka saa kumi na moja na robo, ingawaji nilipata ukinzani mwili kukubaliana akili kwani nilijihisi uchovu na hiyo hutokana na kosa nililofanya la kuchelewa kulala tofauti na muda wangu nilio jiwekea kila siku Nimefanikiwa kuanza na sala na tahajudi huku nikipata lita moja ya maji ya vuguvugu kama utaratibu niliojiwekea.Kisha kufikiria ni mteja gani ninayetakiwa kuwasiliana naye siku hiyo na kisha kuandaa mpango wa mawasiliano. *Kitabuni leo na Tabia za kitajiri cha Dr.Makirita amani-ukurasa wa 124 hadi 133* _Maisha ya kuwa na kiasi_ Moja ya tofauti kati ya masikini na matajiri ni maisha ya kuwa na kiasi, matajiri hawafanyi vitu kwasababu wana pesa ya kufanya bali hufanya kwasababu ni muhimu. Ila masikini wakiwa na fedha wanatamani wanunue kila kitu, anunue nguo,vyombo na kila kitu hata kama siyo muhimu kwake kwa wakati huo. Matajiri wanafahamu madaraka makubwa huja na majukumu makubwa hivyo huwa makini sana sana kwenye matumizi ya fedha zao. Masikini wakipata fedha kila mtu atafahamu kutokana na kukosa kiasi kwenye matumizi yao.Masikini hukasirika kwa vitu vidogo na huwa na furaha kubwa kwa vitu vya kawaida. *Vitu vitatu vya kuvifanya siri kwenye maisha yako* 1.Mahusiano yako ya kifamilia. 2.Hali yako kiafya. 3.Kiwango cha fedha ulichonacho. Matatizo mengi huanzia kwenye mambo haya yanapokuwa wazi kwa kila mtu. Namshukuru mungu nimefanikiwa kukamilisha mambo matano niliyojipangia kuyakamilisha kwenye siku yangu na nimefanikiwa kutuma ujumbe kwa moja ya wateja wangu kumshukuru kwa kuwa nasi na kumuomba aendelee kufurahia huduma zetu. Nashukuru kwa siku hii na usiache kujiuliza swali hili. 'Je kama siku yangu hii ingekuwa kitabu kingesomekaje?' kinyagakelvin162@gmail.com 0763766944/0712161251

Monday 7 June 2021

Kitabu cha leo tarehe 07/06/2021

Habari za wakati huu rafiki yangu. Ni mudaa mrefu umepita sijakuandikia ujumbe wenye mafunzo lakini sasa nitaandika tathimini fupi kwenye siku yangu. *Ujumbewa leo* Wakati unafikiria changamoto ulizonazo tambua na zingine nyingi zipo njiani hivyo ongeza mwendo wa kuzikabiri. Rafiki yangu moja ya faida kubwa ambayo nimeipata kwenye kujifunzani kuchagua kuanza siku kwa ushindi, je wewe rafiki yangu unaianzaje siku yako?Je unaanza kwa kuangalia habari?je unaanza kwa kuperuzi mitandao ya kijamii?kama unaanza siku yako kwa mtindo huo nakupa pole sana Maswali mazuri ya kujiuliza. 1.Ni vitu gani nilivyonavyo vya kumshukuru mungu?viandike kwenye diary yako. 2.Je ni namna ni namna gani unatamani siku yako iwe?malengo ya siku.Hakikisha unaipangilia siku yako. usipofanyahivyo wengine watakutumia kwenye siku hiyo kwa manufaa yao. 3.Panga ni namna gani utaongea na mteja wako, kama umeajiliwa boss wako ndio mteja wako. 4.Ni kitabu gani utakwenda kusoma kwenye siku unayoiendea? Mimi leo nimeweza kukamilisha yale niliyopanga kwa zaidya asilimia 90.Pamoja na ushindi huo zipo changamoto kadhaa nimezipitia. 1.Wakati unapanga muda wako tambua na wengine wameandaa mipango yao kwa kutegemea wewe?Hivyo jiandae kukabiliana na hilo. 2.Zipo tabia mbaya kama kukasirishwa na watu kwa kutaka wawe kama vile unavyotaka wewe, wafanye vile unavyotaka wewe. Kuwa na mtazamo huu ni kujinyima furaha bilasababu. Asante sana rafiki yangu Kinyagakelvin162@gmail.com 0763766944/0712161251

Monday 22 March 2021

01/100 Jione Uko Kitandani Ukikabiliana Na Kifo.

Habari za wakati huu mpendwa wangu,hamasa ni kiungo muhimu sana kwa maendeleo yetu,naomba upokee mfululizo wa mambo 100 ya kufanya ili kujitengenezea hamasa mwenyewe pale unapohisi kukata tamaa kutoka kitabu kinachoitwa 100 WAYS TO MOTIVATE YOURSELF kilichoandikwa na Steve Chandler...... Hebu rafiki yangu pata picha upo kitandani ukikabiliana na kifo,wapendwa wako wanakuja wakilia na kumuomba mungu asikuchukue,ona watoto,mke au mume wako wakikulilia ukiwa umeshakufa. Kisha amka ukifahamu muda wowote hilo litatokea na ona nafasi uliyoipata leo ni ya mwisho.Je utaendelea kughailisha mambo yako mazuri uliyopanga kufanya? Bob Dylan aliimba 'he who is not busy being born is busy dying'. Rafiki wakati mzuri wa kupambana ni sasa usisubiri wakati wa majuto na kusema ningejua,fanya sasa ujishukuru baadae. Asante na nikutakie siku njema. wakikulilia

Sunday 14 February 2021

Kuna Mengi Nimejifunza Kupitia Barua Hii Ya Kumi

Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kukupongeza kwa namna unavyojitoa kutuelimisha,hakika nimejifunza vitu vingi sana kupitia barua hii ya kumi na baadha ni kama ifuatayo. *Acha kutoa sababu toa matokeo* Imekua ni kitu cha kawaida pale tunaposhindwa kutekeleza majukumu yetu kwa wakati kutoa sababu na kutaka watu kutuamini kwa sababu hizo. Kwanza kabisa nianze kwa kukupa pole kwa kuondokewa na mkwe wako,lakini pamoja na hilo kwangu na kwa unayesoma hapa tungetumia sababu hiyo kutokamilisha majukumu yetu na kuona ni sababu ya msingi,ni kweli ni ya msingi lakini hapo ndio panapotofautisha kati ya washindi na washindwa. *Ushirikina,dini na sayansi* Hapa kocha umefanya mapinduzi makubwa sana.Kwanza kabisa umeonyesha kwa mifano ni namna gani dini na ushirikina kwa sehemu zinatulazimisha kuamini vitu bila kuhakikisha usahihi wake wakati sayansi inatupa uhalisia wa jambo kwa kurithbitisha.Hakika tunapaswa kuwa makini sana na dini zetu maana tusipoangalia tunakuwa sawa na washirikina. *Kila dhambi ni zao la ushirikiano* Dhambi ni makosa ambayo mtu anafanya tena mara nyingi kwa makusudi kabisa.Sasa kwa hili la covid 19 ni kweli kabisa sehemu kubwa ya lawama ziende kwa serikali lakini kwenye hili hata sisi tuna mchango wetu. kwanza kabisa ni ushabiki wa mambo yasiyo na tija kwetu na kupuuza ukweli ambao uko wazi,jana kwenye jumuiya daktari wa kcmc katupa elimu kuhusu ugonjwa huu lakini cha kushangaza leo kanisani watu wanarudia makosa yaleyale eti serikari haijatangaza hivyo corona hakuna.Sisi tunaotafuta maarifa sahihi tukawe mfano wa kuigwa.Asanteni wote.

Saturday 23 January 2021

Unaitumikia fedha au fedha inakutumikia?

*Je maisha yako yanaweza kwenda kama kawaida hata kama hutafanya kazi moja kwa moja?* Rafiki yangu maswali ni njia nzuri sana ya kujifanyia tathimini,karibu ujifunze ili fedha akawe mtumwa kwako na kukufanyia kazi...... Kitu unachopaswa kufahamu ni kwamba kuna siku hutaweza kufanya kazi ili upate fedha kama sasa,pengine kwasababu ya uzee au ulemavu wa viungo ambavyo leo unavyo lakini kesho hutakua navyo kwasababu kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.Hapo ndio unahitaji kuanza maandalizi ya fedha kuwa mtumwa wako. Njia pekee ya kuweza kuifanya pesa kutufanyia kazi ni kuitumia fedha unayopata sasa kama mbegu kwa kuiwekeza. Uwekezaji ni pale fedha unayoipata inapokufanyia kazi badala ya wewe kuifanyia kazi kama unavyofanya sasa. Rafiki utakua shaidi kwamba asilimia kubwa ya wastafu hufa mapema baada ya kustafu kwasababu nguvu za kufanya kazi hawana na pesa zinakua haziwezi kukidhi mahitaji yao,hivyo kama hutojifunza sasa namma ya kuwekeza jiandae kwa maisha ya mateso wakati nguvu na uwezo wa kufanya kazi utakua huna. Faida nyingine ya uwekezaji unaipata kwa kustafu kazi ya kuajiriwa na kujiajiri kabla ya umri wa kisheria wa kustafu haujafika. Ninafahamu nikitaja neno uwekezaji unawaza mamilioni ya fedha lakini ukisoma kitabu cha *elimu ya msingi kuhusu fedha* jambo la msingi kwenye uwekezaji ni KUANZA MAPEMA NA KUWEKEZA KILA WAKATI. Angalia wafanyakazi wanapolipwa mafao yao baada ya kustafu,lakini fedha hiyo ni kidogo ukilinganisha na namna ilivyowekezwa na kuzalishwa. Rafiki kwa leo ni hayo nenda kayafanyie kazi. Kinyagakelvin162@gmail.com 0763766944