Thursday, 21 May 2020

Anza asubuhi yako na S.A.V.E.R.S.....



Rafiki bilashaka umeanza siku yako ukiwa na utulivu kabisa na unaomba mungu siku yako iendelee na utulivu huo, uko Sawa lakini upande mwingine jiandae na watu wasio na shukrani, wenye kukukwaza na kukuvuruga ili pale wanapojaribu kukuvuruga usipatwe na mshituko wowote na hali hiyo itakupa hekima ya hali ya juu kukabiliana nao kwa kujiambia sitajibizana nao wala kugombana nao, karibu tuendelee........

Rafiki na ndugu yangu, linapokuja swala la asubuhi Kila mmoja wetu ana utaratibu wake, wapo wanao amka na kuanza na kushika simu zao na kuperuzi mitandao ya kijamii, wapo wanao anza asubuhi zao kwa kusikiliza habari magazetini, wapo wanaonza asubuhi zao kwa kubishania michezo na Kila namna nyingi kadri ya mapenzi ya mtu, pengine kwa kuanza siku yako na utaratibu wako huoni kama kuna tatizo lolote na unaweza kushangaa kwanini ifike sehemu nishauriwe ni kwa namna gani niianze siku yangu,rafiki kwenye ulimwengu huu wa habari kuna Kila habari na ni wewe ndio mwamuzi wa kipi unapaswa kusikia na kipi huhitaji, lakini kile unacholisha akili yako ndicho utakachovuna,kama Kila siku unalisha habari hasi za kukatisha tamaa au za kuhuzunisha ndivyo utakavyoyaishi maisha yako, na habari nyingi za mitandao ya kijamii ni hasi kwa zaidi ya 90%.Habari zote muhimu unaweza kuzisikia bila hata kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii, siku zetu ni mfano wa maisha yetu, tunapokuwa vijana tunakuwa na nguvu kubwa ya kazi lakini tukishafika uzeeni tunakuwa hatuna nguvu hizo, sasa unapoanza siku asubuhi unakuwa na nguvu kubwa sana na inapofika jioni nguvu hizo upunguwa hivyo ukianza na habari hasi unakuwa umepoteza nguvu zako kwa haraka sana, hivyo hapa chini tunakwenda kujifunza kanuni bora ya kupangilia asubuhi yako na ukajikuta hupotezi nguvu zako na unafanya mengi ambayo usingeweza kufanya kama ungechaguwa kuendelea kuanza siku na habari za mitandao.

S.E.V.E.R.S
Wiki iliyopita nilitumiwa kitabu na rafiki yangu Dr.Raymond Mgeni,kitabu hicho kinakwenda kwa jina la MIRACLE MORNING FOR WRITERS na kimeandikwa na Hal Elrod&Steve Scott,mwandishi kaonyesha anakiandika kwa ajili ya waandishi lakini nina amini yaliyomo humu yanamsaidia Kila binadamu mwenye kujuwa kusudi la maisha yake. Hatua ya kwanza tutakwenda kuzielezea harufi hizo moja baada ya nyingine na maana zake.

1.Herufi 'S'
Herufi hii inasimama kwa neno SILENCE, watu wengi wanaanza siku kwa kelele, mitandao ya kijamii,habari ni kelele. Unapoanza siku yako kwa ukimya, pengine ukatumia dk 5 kumshukuru mungu na dk 10 kutuliza akili yako,kuwa na utulivu mkubwa kiasi kwamba una uwezo wa kuyasikiliza mapigo yako ya moyo, wazungu wanaita Meditation, hii itakuondolea stress na itakupa utulivu mkubwa sana, watu wengi hukosa kabisa muda huu na ndio maana mambo yao muhimu wanayakumbuka wakiwa mariwatoni au bafuni kwani ndio sehemu pekee wanapokuwa peke yao. Hivyo rafiki Tenga muda wako asubuhi sana Kila siku kabla ya kufanya chochote na fanya tahajudi(meditation) yako.

2.Herufi 'A'
Herufi 'A' inawakilisha neno 'AFFIRMATION'.Neno hili linakutaka uwe na maneno ambayo utayasema na yanakupa nguvu ya kuendelea na kile unachohitaji, pengine umechoshwa na madeni na unataka kuachana nayo. Ukayaandaa maneno ambayo unayasoma. Mfano.Nimekuwa kwenye utumwa wa madeni kwa kipindi kirefu na nimechoshwa na utumwa huu, kuanzia Leo siwezi kukubali kuendelea na hali hii na nitahakikisha namaliza madeni yote, niko tayari kushindia uji lakini niondokane na utumwa huu. Baada ya kutamka maneno hayo Kila siku asubuhi sidhani kama utashindwa kuondokana na madeni. Hivyo unaweza kuweka maneno yoyote kwa kile unachohita na Nina amini utafanikiwa.

3.Herufi 'V'
Herufi 'V' inasimama kwa neno 'VISUALIZATION'. Hapa unatengeneza picha ambayo iko kwenye akili yako, pengine kwa mfano wa mtu mwenye madeni hapo juu, anaweka picha kwamba baada ya muda fulani atakuwa hana deni, ataanza kuwekeza akiba na atafunguwa malengo account na anaona amekuwa mfanyabiashara mkubwa, anamiliki nyumba na mengine mengi, kuwa na picha ya kile unachotamani kunakupa nguvu ya kuchukuwa hatua.

4.Herufi 'E'
Herufi 'E' inasimama kwa neno 'EXERCISES' rafiki mazoezi ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu, mwili wenye afya ni mwili wa mazoezi, tumia dakika si chini ya 10 kufanya mazoezi ya viungo, kimbia, luka kamba na hili litaupa mwili nguvu ya kupambana na Afya ya mwili na hilo ndio mwanzo wa mafanikio mengine, kwani afya kwanza mengine ziada.

5.Herufi 'R'
Herufi hii inasimama kwa neno 'READING',tengeneza utamaduni wa kusoma, ukiweza kusoma kurasa 10 kwa siku na hili litakufanya ulishe akiri yako, kwani mwili wenye chakula usio na chakula kwenye akili yake ni mwili usiokuwa na macho, kwenye vitabu kuna utajiri mkubwa sana.

6.Herufi 'S'.
Inasimama kwa neno 'SCRIBING'ambalo lina maana Sawa na neno 'WRITTING',rafiki kuandika ni muhimu sana, unaweza kuandika ratiba ya majukumu yako ambayo unakwenda kuyatekeleza kwenye siku yako, ikiwezekana andika na wale utakaopaswa kuwasiliana nao kwenye siku unayoiendea, andika matumizi unayotarajia kufanya kwenye siku yako.

Rafiki kwa kuanza na mtililiko wa neno S.E.V.E.R.S Kwenye siku yako utakuwa mtu mwenye hamasa sana kwenye siku unayoiendea na asubuhi yako itakuwa tulivu sana, ukiamka masaa mawili au moja kabla ya kwenda kwenye shughuli zako na kutekeleza haya hakika utakuwa umeanza kwa ushindi mkubwa, nenda kayaishi haya kwenye siku yako na utanishukuru, mwanzo hautakuwa rahisi hivyo pambana mpaka ufanikiwe kwenye hili.

Kinyagakelvin162@gmail.com
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944

No comments:

Post a Comment