Tuesday, 26 May 2020

Matatizo yako kifedha yanasababishwa na changamoto hizi mbili......



Rafiki hongera sana kwa kuwa na ujasiri wa kuendelea na mipango yako mizuri pamoja na changamoto unazopitia, hiyo ndio maana ya ushindi, kuendelea kufanya bila kuchoka na hapo unakuwa shujaaa halisi.

Kutoka kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON alikuwepo mtu mmoja aliyeitwa Arkad, mtu huyu alikuwa na utajiri mkubwa sana, siku moja rafiki yake wa utotoni alimtembelea na kumuuliza alifanyaje mpaka akaupata utajiri huo? Wakati anakumbuka hakutoka kwenye familia ya kitajiri labda pengine anaweza kuwa ni Mali za kurithi?ndipo Arkadi anamjibu kama mpaka Leo unatengeneza fedha kwa ajili ya chakula na mahitaji madogo madogo pekee basi una matatizo haya mawili, hivyo nataka kushare na wewe matatizo hayo mawili hapa chini.

1.UMESHINDWA KUJIFUNZA SHERIA ZA FEDHA
Pamoja na umuhimu wote wa fedha kwenye maisha yetu lakini elimu hii haifundishwi mashuleni na hapa ndio kunafanya idadi ndogo sana kuzijuwa sheria hizo.

2.UZIFUATI SHERIA HIZO
Wapo wengi wanafahamu sheria chache za fedha lakini kwa makusudi kabisa wanazivunja, watu wanafahamu kabisa kwamba hawatakiwi kutumia zaidi ya kipato chao lakini wanaamua kutumia zaidi na kuishi hivyo kwa maisha yao yote.

Hayo ndiyo matatizo mawali ambayo pengine na wewe rafiki yangu unayo, sasa pengine unajiuliza utapata wapi elimu hiyo wakati mashuleni hawatufundishi?

Kwenye kitabu hiki kupitia maongezi ya tajiri Arkadi na rafiki yake, Arkadi anatuambia aliajiriwa kama mwandishi na alikuwa akiandikia watu,siku moja alikuja Tajiri mmoja ambaye alimtaka Arkadi amwandikie sheria ya Tisa ambayo ilikuwa ndefu na Arkadi alishindwa kuikamilisha kwa wakati aliotaka Tajiri yule aliyeitwa Algamashi, Mtu yule alikasilishwa lakini Arkadi hakuogopa ndipo akamwambia kufika kesho itakuwa imekamilika ila nataka unifundishe ni kwa namna gani naweza kuwa tajiri kama wewe? Ndipo mzee tajiri anamwambia kamilisha kazi niliyokupa nitakufundisha hata na hivyo nimeshakuwa mzee na sasa nitafurahi vijana wakijifunza kwa wazee, anasema maisha ya ujana ni Sawa na Mwanga wa kimondo lakini Busara za wazee ni Sawa na nyota.

Rafiki tutaendelea na simulizi hii wakati ujao lakini nina imani yapo uliyoondoka nayo, Je mtaani kwako hakuna wazee kama Algamashi ukawatafuta wakakuambia ni kwa namna gani sheria za fedha walizo ziishi zimewafanya wakafika hapo? Au tunawaacha wafe na utajiri wao vichwani mwao bila kutuachia?

Asante sana rafiki na uwe na siku njema.

Kinyagakelvin162@gmail.com
Bonyeza kiungo;
https://kinyagakelvin.blogspot.com

Hapo utajifunza masomo yaliyopita kama uliyapoteza.
0763766944

No comments:

Post a Comment