Sunday, 24 May 2020

Vitu vyote duniani vina kasoro ila siyo vibaya.....



Hebu mfikirie mtu anayependa kile anachofanya kwa moyo wake wote, akili na nguvu zake,halafu, mtu anayewapa watu nafasi ya kukosea na mwepesi wa kusamehe na anasema ukweli kwa Kila kitu hata kama utamuumiza na yeye pia, ona mtu huyu alivyo na maisha ya furaha na Amani moyoni mwake, chagua kuishi hivi Leo na siku zote kama unataka......

Leo tutaangalia mtazamo wa kuona vitu kwa UBAYA, pengine wapo watu waliokuumiza sana,wezi na wengine wengi waliokutendea ubaya wa Kila namna, kuna mtu anaweza kukushawishi kwamba watu hao siyo wabaya ukamuelewa? Lakini leo nataka kukuambia mtazamo wowote ulio nao kwenye watu au vitu hakuna ubaya wowote bali kuna kasoro.

Unapoona vitu au watu kwa mtazamo wa kasoro unajipa nafasi ya kutokuwa na chuki na chochote na hasira na yeyote yule kwani hata wewe unakasoro zako, kwani hata mtu anayeonewa ni kwa sababu ya upofu wake ambao ni kasoro ndio maana wengine wanaona kwa niaba yake na pale atakapogundua kasoro yake hatokubali kuonewa na yeyote.

Hebu fikiria mwizi kavunja na kakuibia Mali zako, ukiwaza kwa ubaya unaweza kuona chuki dhidi ya mwizi huyo ukikutawala na bahati mbaya usimuone na siku nyingine ukaibiwa tena kwani hata mwizi huyo anaona kasoro zako na ndio maana anakuibia Kila siku lakini pale unapoona kasoro zilizopo zaidi kwako unawasaidia hata wanaokutendea ubaya.

Ukichukulia mfano wa mwizi hapo juu, kwa mtazamo wa kasoro zilizopo upande wako unaanza kuona pengine ni geti lako linashida,pengine unahitaji kuweka ulinzi kwenye eneo lako au uzembe wowote ambao utakufanya uchukuwe hatua. Je umetapeliwa? On a kasoro zako na lekebisha, acha kukimbilia kulaumu wengine kabla ya kuona kasoro zako,wengine wanapokukosea wanakuonyesha kwamba kuna vitu vina kasoro na unapaswa kurekebisha.

Pengine kwa hayo machache utakubaliana na Mimi kwamba hakuna kitu chochote kibaya bali kuna kasoro na jifunze kuona wema kwenye Kila ubaya, Asante najumapili njema.

https://kinyagakelvin.blogspot.com
Email yangu;
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944

No comments:

Post a Comment