Saturday, 2 May 2020
Ubongo(Akili)+Vitabu vinne+Kocha+Menta+Porojo vitakuvusha........
Habari za wakati huu mwanamafanikio mwenzangu, bilashaka unaendelea kuishi bila hofu kwasababu unafahamu hofu haina msaada wowote, lakini pia unajitaidi na vile vilivyo ndani ya uwezo wako ili kujikinga na janga linalotukabiri, karibu kwenye ukurasa huu tujifunze baadhi ya vitu ambavyo Nina amini ukivisoma na kuvifanyia kazi utayafikia mafanikio yoyote unayoyahitaji, karibu tuwe zote mpaka mwisho.......
AKILI
Rafiki unahitaji muunganiko wa vitu vingi ili uweze kufanikiwa, hakuna kitu kimoja ambacho mtu yeyote atakushauri ukifuate na ukafanikiwa, lakini haimaanishi basi Kila kitu utakachoambiwa ndio sahihi hivyo unahitaji akili timamu ya kuchuja yale unayoona na kuyasikia kuhusu mafanikio, kitu unachopaswa kufahamu ni kwamba akili haipatikani shuleni na hakuna shule ambayo inafundisha akili hivyo usihusianishe mafanikio uliyopata shule au kutofanya vizuri darasani ndio sababu ya kutofanikiwa, wapo watu wengi waliogundua vitu vikubwa bila ya kwenda shule, Abraham Lincoln, Harry Truman,George Bernard shaw mtu aliyeshinda tuzo ya Nobel aliacha shule akiwa na miaka 16,John Major aliyekuwa waziri Mkuu wa uingereza na wengine wengi wenye majina makubwa na wamefanya mengi wakati elimu zao ni za kawaida sana hivyo usitumie kigezo cha kutokwenda shule au kufanya vibaya kwenye masomo yako kama sababu ya kushindwa, shule ina mchango wake lakini siyo sababu ya kutofanikiwa, hivyo akili ni moja ya nyenzo muhimu kuwa nayo.
VITABU VINNE
Rafiki kama kweli unahitaji kufanikiwa ipo tabia ambayo lazima uwe nayo, tabia hiyo ni ya kusoma vitabu, kwenye vitabu kuna Kila mafanikio na utajiri unao hitaji, unaweza kuanza kuuliza mbona kuna vitabu vingi sana je nianze na vipi?,rafiki ni kweli kuna utitili wa vitabu vingi sana na usipokuwa makini unaweza usifahamu unataka nini kwenye vitabu, lakini vipo vitabu vinne ambavyo kocha wangu alinishauri ni lazima nivisome kama kweli nataka kufanikiwa, nimesoma vitabu vingi sana lakini vitabu hivi vinne Nina kuambia visome na ukivimaliza rudia Mara nyingi uwezavyo huku ukifanyia kazi yale unayo jifunza, vitabu hivyo ni THINK AND GROW RICH- humu utaona namna fikra zako zinavyochangia wewe kufanikiwa au kushindwa na kwanini kushindwa au kufanikiwa sababu ni wewe na siyo mtu yeyote yule,Kitabu cha pili ni THE RICHEST MAN IN A BABYLON-Hapa utapata historia ya mji wa babeli na mtu tajiri aliyesababisha babeli iwe na nguvu duniani wakati ni eneo lililokuwa jangwa, kuna matajiri wengi wamekuzunguka je ulishawauliza walifanya nini wakafika hapo? Basi kitabu hiki kitakupa Kila kitu kwenye safari yako ya matumaini, Kitabu cha tatu ni RICH DAD-POOR DAD-Hapa utakutana na baba wawili mmoja msomi sana lakini masikini na mwingine ana elimu ya kawaida lakini ni tajiri na kipi kilisababishwa na hayo yote na nini utajifunza kwa wababa hao, vitabu vyote hivyo juu vimeandikwa kwa kingereza, kama kingereza kwako ni tatizo karibu ujiunge na kisima cha maarifa utapata uchambuzi mzuri sana kwa lugha ya kiswahili, kitabu cha nne na cha mwisho ni kitabu kilichoandikwa na Mtanzania kinaitwa ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA-Kitabu hiki kimefanyiwa utafiti kwa kutumia nchi yetu ya Tanzania na kina Kila msingi muhimu wa fedha na kimeandikwa kwa mifano ya nchi yetu, wapi uweke fedha yako ili ikufanyie kazi na makosa yote unayofanya kwenye fedha, ukivisoma vitabu hivyo vinne na usifanikiwe baada ya kufuata yaliyopo humo nina neno nzuri la kukuambia, huna akili Timamu, rudia Mara tatu kujiambia sina akili timamu.
KOCHA
Rafiki nikisema kocha si maanishi uwe mchezaji wa mpira wa miguu ndio uwe na kocha, kocha ni mtu ambaye changamoto zako ni fursa kwake, mfano wewe una changamoto inayokusumbuwa unamshirikisha halafu bila kusita anakuambia ufanye nini ujikwamue na changamoto uliyo nayo, Lakini kuna mtu unamkosa kwenye maisha yako na mtu huyo siyo adui Bali rafiki atakayekuambia unakosea na kukukalipia unavyofanya kinyume na kile unachopaswa kufanya ili ufanikiwe, siyo rahisi kupata rafiki huyu ila ukimpata utakubaliana kwamba ni kiungo cha kukupeleka kwenye ndoto zako. Ukihitaji mtu wa namna hii tuwasiliane.
MENTA
Pamoja na kwamba tayari una Kocha, mtu ambaye atakusimamia kwa ujumla kwenye Kila kitu bado utahitaji mtu aliyebobea kwenye kile unachotaka kukifanya, pengine unataka kubobea kwenye kilimo basi tafuta menta wako kwenye kilimo ambaye ana uzoefu kwenye kilimo, biashara, sheria,fundi na mengine mengi, sifa ya menta mzuri lazima akue kwenye kile anachofanya siyo kukifanya kwa muda mrefu bali Kila siku anapiga hatua za juu kwenye kile anachofanya.
POROJO
Rafiki mwisho kabisa unachohitaji ni porojo za wengine, naweza nisieleweke kutumia neno porojo lakini usinielewe vibaya, baada ya kufuata yote yaliyopo hapo juu basi kuna mengine mengi utayasikia kwa watu wanao kuzunguka, huwezi,unajisumbua bure, unajitesa bila sababu, bahili na ushauri mwingi usio kuwa na tija lakini kwakuwa umeshafuata yale yote yaliyo hapo juu kwako utajuwa hayo unayoshauriwa ni porojo tu, sikuambii ukabishane na watu bali nakuambia ili ukikutana na mengine njee ya yote hapo juu au yanayokwenda kinyume uyapuuze na porojo zingine utazisikia na kuona ni msingi wa kile ulichojifunza na utakiongezea, kama hutofuata nilichokushauri Kila mtu atakuwa mshauri wako na utachanganyikiwa na hutofika popote.
HABARI NJEMA
1.Nitakuletea makala kutokana na akili nilizo nazo,vitabu hivyo vinne,kocha na porojo zilizopo ili ukae nazo mbali, Kila mwisho wa wiki utapata mkusanyiko wa mambo hayo.
2.Share na wengine andiko ili na jiandae kwa maandiko yanayofuata.
3.Endelea kutembelea blog yangu kwa kubonyeza kiungo hiki https://kinyagakelvin162.blogspot.com kuna makala nzuri kwa ajiri yako.
Makala hii imeandikwa na Kelvin Kinyaga, mwalimu na mwana kisima cha maarifa asiye na shaka yeyote ya kufanikiwa kwani ni muda tu ndio unasubiriwa. Wasiliana naye kwa No 0763766944 au email Kinyagakelvin162@gmail.com
Asante sana,hifadhi andiko hili na mtumie Kila anayekuomba ushauri, usinishukuru kwa andiko bali fanyia kazi yalipo kwenye andiko,nakupenda Daima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment