Saturday, 30 May 2020

Haijarishi unapitia nini hupaswi kuacha kutekeleza mambo haya manne.....



Habari za wakati huu rafiki yangu ninachoamini ni kwamba kadri siku zinavyosogea ndivyo tunavyokikaribia kifo, huna haja ya kuogopa kwani kufa ni hakika ila siku zote ogopa kutokuishi, maana unaweza kuwa hai lakini huishi bali unaigiza kuishi, muda ni mchache sana Fanya yaliyo sahihi.......

Rafiki yangu huwa kuna siku unakuwa na nguvu sana na hamasa ya juu ya kutekeleza majukumu yako, lakini wakati mwingine unakuta unajihisi uchovu, unahisi kukata tamaa, pamoja na vyovyote vile unavyojisikia wanafalsafa wanatushauri mambo haya manne hatupaswi kuacha kufanya kwasababu yoyote ile.

COURAGE,TEMPERANCE,JUSTICE AND WISDOM

COURAGE (UJASIRI)
Rafiki huwa tunakosa ujasiri kwasababu ya mambo ya nje, pengine ni shida imekuandama ukakosa ujasiri wa kusimamia ukweli, usilazimike kufanya chochote kile kwasababu yeyote ile, kuwa jasiri siku zote, tenda wema na kataa ouvu hata kama utakuumiza, jiambie siku zote kwamba haijarishi napitia yapi nitaendelea kuwa jasiri.

TEMPERANCE(HALI YA JOTO)
Ni kawaida kwetu sisi binadamu pale tunapopitia magumu au kuwa na shida fulani tunakuwa na hali ya unyonge, tunakuwa baridi kwasababu tumepata matokeo ambayo hatukuyatarajia,lakini hilo halina utatuzi kwetu, haijarishi Jana ulishindwa, amka Leo na jiambie ninakwenda kupambana tena, usikubali siku moja ikaharibu siku zingine nyingi, uliferi darasani ondoa unyonge na pambana.

JUSTICE (HAKI)
Kuwa mtu wa haki siku zote za maisha yako, usiwatendee wengine kile ambacho usingependa kutendewa, hakuna mazingira yoyote yatakayokufanya usiwe mtu wa haki, ili litakufanya uwe na nguvu siku zote, Mara nyingi usipotenda haki utakuwa umechaguwa upande usio sahihi.

WISDOM(HEKIMA)
Hiki ni kitu kigumu sana kukitekeleza, lakini kwa kujifunza Kila siku kwenye maisha yetu na kubadilika hakika tunaweza fikia kiwango cha juu sana cha hekima,Kila mtu anatamani sana kuwa na hekima ila niwachache sana wana hekima, kuwa msikilizaji zaidi, usihukumu wengine na kuwa mwepesi kusamehe usiwe mtu wa chuki na visasi.

Basi rafiki ujasiri,kuendelea kupambana bila kuchoka,kuwa mtu wa haki na hekima ni vitu unavyopaswa kuvifanya siku zote kwenye maisha yako haijarishi unayapitia yapi na hakika utaufikia utosholevu wa juu sana kwani vitu hivi ni kama mbegu ambayo wewe mpandaji ndio utavuna matunda kwenye mbegu hizo nenda kayaishi haya.

Kinyagakelvin162@gmail.com

My Email;
https://kinyagakelvin.blogspot.com

0763766944/0712161251
Asante.



No comments:

Post a Comment