Tuesday, 19 May 2020

Hatua sita za kufuata ili kujipatia uhuru kwenye fedha......



Bila shaka neno asante ndio neno linalopaswa kuwa la kwanza kutamkwa kwenye Kila asubuhi yako, kwani kuishi na kuiona siku ni bahati tu na upendeleo mkubwa hivyo kupoteza muda ni kauli inayotumiwa na watu waliozoea kuchezea shilingi kwenye tundu la chooni, sina shaka na unayesoma hapa kwamba unafahamu umuhimu wa muda na kamwe hupotezi kwa mabishano,masengenyo wala kufanya yale yote yasikuwa na tija au kukuongezea hekima, kwani kwa kufanya hivyo ni kuchagua kupoteza kabla hata hujapata.

Rafiki Leo tutajifunza hatua sita unazopaswa kuzifuata ili kufikia Uhuru kifedha.....,hatua hizi tunazipata kutoka kwenye kitabu cha THINK AND GROW RICH karibu tuwe sote mpaka mwisho wa makala hii na hutabaki kama ulivyo.

1.Unahitaji kiasi gani cha fedha?
Rafiki utakubaliana na Mimi kwamba akili zetu zinajisukuma kwa kadri ambavyo tunazishughulisha,wengi tumezoea kutafuta fedha kwa ajili ya matumizi muhimu ya Kila siku na tukipata zaidi ya hapo tunazitumia vibaya na kisha kurudi kwenye maisha yetu tuliyozoea, hivyo kwenye kitabu hiki tunashauriwa kujiwekea kiwango ambacho tunaweza kujisukuma na kukipata lakini kisiwe kikubwa cha kutukatisha tamaa,tatizo siyo kuweka kiwango kikubwa na kushindwa kukifikia bali tatizo ni kujiwekea kiwango kidogo na kukifikia, mwandishi mmoja amewahi kusema.

2.Je ni kitu gani upo tayari kulipa ili uweze kufikia kiwango hicho?
Hakuna kitu ambacho utakipata bila ya gharama, lazima uwe tayari kugharamia ili uweze kupata unachotaka, pengine muda mwingi unajihusisha na kuangalia Tv,pengine ni kupumzika ndio kitu unapenda,pengine kukaa bila kufuatilia maisha ya wengine, pengine maisha ya kujinyima hukuzoea, haya yote ni baadhi ya gharama ambazo lazima uwe tayari kuzilipa, mwandishi mmoja amewahi kusema ukitaka kufanikiwa lazima uwe tayari kukataa vitu unavyopenda na kuchaguwa vitu usivyovipenda vinavyokufanya uwe bora.

3.Amua na Panga tarehe ambayo unataka uwe umeshakifikia kiwango hicho.
Kocha Wangu anapenda kusema chochote kisicho na muda wa kukitekeleza basi hakiwezi kutekelezeka, hivyo huwezi weka kiwango unachotaka kukifikia halafu usiweke ni lini unatakiwa kuwa umeshakikamilisha.

4.Tengeneza mpango wa kukifikia.
Lazima uwe na mkakati wa kukifikia, pengine nitaanzisha biashara ya chakula, au kuuza vitafunwa au nitatoa kwenye mshahara Wangu, kwa wiki nitatakiwa niwe nimepata 10000 na kwa mwezi 40000 na kwa mwaka ni 480,000. Bila kuwa na mpango kamili hiyo inabaki kuwa ndoto kupata kiasi hicho.

5.Kuwa na Maelezo mafupi yanayotaja kiasi cha fedha unachohitaji.
Mfano. 480,000 iwe imepatikana mpaka kufikia tarehe 01/01/2021 kutokana na biashara ya vitafunwa ninayofanya na Kila wiki lazima iwe imepatikana Tsh 10000 na kwa mwezi 40,000. Hivyo siku zote utakuwa unapambana kufika hapo.

6.Yasome yote uliyoandika hapo juu Kila siku Mara mbili.
Basi hatua ya mwisho ni kuhakikisha Kila siku asubuhi unasoma kile ulichokiahidi mwenyewe na unataka kukifikia, pia jioni kabla hujalala unapitia tena na kujipima kama unaendea kupata au la!,hivyo Jua liwake mvua inyeshe hutokubali kujipa sababu kwanini hujapata kiasi hicho.

Hivyo rafiki ndivyo mwanzo wako wa kufika unakotaka kufika unavyoanza kufanyiwa kazi, lakini ukijiambia unahitaji fedha nyingi bila kujuwa unazipataje na lini ikifika uwe umezipata na mkakati upi unao wa kufikia lengo lako unakuwa umechaguwa kushindwa, na pindi utakapokifikia kiwango hicho unajipongeza na kupanga kiwango cha juu zaidi na kufuata hatua hizo sita.

Asante sana rafiki na nikutakie siku njema na kazi njema pia.

https://kinyagakelvin.blogspot.com
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944.
#Tuvuke pamoja


No comments:

Post a Comment