Friday, 29 May 2020

Misimamo yako isiyoyumba inavyokuyumbisha......



Katika kitu ambacho ni Zawadi kubwa ambayo unaweza kuitumia vizuri na kufika mbali basi ni upweke,kuna wakati unaweza on a dunia imekutenga, marafiki, shida zimekuandama na huoni mbele, huu ndio wakati mzuri sana ambao uliukosa pale ulipokuwa umezungukwa na kelele za marafiki fake ambao sasa wamekukimbia na hapo unakuwa na utulivu ambao ni nguvu ya kukusogeza unakotaka kufika, pengine ni rafiki zako waliojuwa mipango yako ndio walikufelisha na sasa hawapo, acha kulalamika tumia upweke kufika kule unakotaka kufika...........

Rafiki yangu pengine neno MSIMAMO ni neno ambalo Kila mtu anatamani kuonekana analiishi kwenye maisha yake, lakini nimekutana na wengi ambao misimamo imewafikisha pabaya, msimamo ni kitu kizuri lakini lazima uwe makini na misimamo uliyonayo, Miaka ya nyuma kidogo nilijiwekea misimamo mingi sana, sitaki kuonewa na Niko tayari kufa kuliko mtu kunionea, nitadai haki yangu mpaka niipate na mengine mengi, rafiki yangu mmoja akaniuliza iko wapi ile misimamo yako? Leo hakuna ongezeko lolote kwenye mishahara yetu lakini hujawahi funguwa mdomo kwenye hilo kulikoni?

Kwanza kabisa niseme Happy birthday kocha Aman, Jana ilikuwa kumbukizi ya kuzaliwa kwako na leo kama kawaida yako huwa ukiandika makala inayohusu siku yako ya kuzaliwa huwa unapinduwa fikra za wengi sana, kama mtu alikuwa anafikiria kwenda magharibi unampeleka mashariki, asante kaka Raymond kumfanya atuandikie makala kwenye siku yake ya kuzaliwa na makala ile imefanya niandike misimamo wakati mwingine inatuyumbisha.

Hebu fikiria kama kocha angeendelea kuweka kuweka msimamo wa kutotibu ni wangapi ambao wangekosa huduma yake? Hiyo yote ni matokeo ya kutokuwa na misimamo isiyo yumba, baada ya kutathimini makala ile nimeondoa misimamo mingi ambayo nilikuwa nayo na naanza kujiona nimetoka kifungoni.

Mwaka 2024 Tarehe 01 mwezi wa sita ni tarehe ambayo nilikuwa na msimamo nayo kwenye kazi ninayofanya, baada ya kusoma makala ya kocha nimeboresha wazo langu kwa kuregeza msimamo Wangu, Kwa ufupi tangu 2018 nimekuwa nikipunguza utegemezi Wangu kwenye mshahara kwa asilimia 10 na ikifika tarehe hiyo kwa msimamo wangu natakiwa kuwa nina utegemea mshahara kwa chini ya asilimia 50 na asilimia hiyo 50 kuiwekeza.Sasa ninaongeza kiwango cha kuto utegemea mshahara kufikia 20 kila mwaka ili ikifika tarehe hiyo niwe siutegemei mshahara wangu moja kwa moja kama sasa ila Sitoondoka kwenye Ajira kama nilivyopanga ila nitawekeza zaidi kwenye utowaji elimu bora kwa wanafunzi na nataka kuionyesha jamii kuwa mwalimu siyo dhambi na na wala siyo tiketi ya kuwa masikini bali kutumia fikra zetu vizuri kusaidia wengine, maana niliamini huwezi endelea kuwa mwalimu na kuwa na utajiri, nataka niondoe dhana hiyo kwa kubaki kwenye kada ya ualimu na lazima niwe na utajiri ili kujenga walimu wenye wito wengi na siyo walimu wengi wanao ingia kwenye kada hii ili kupunguza stress na kutoa elimu ya hovyo kwa jamii, nitahakikisha naanzisha harakati za kubadili mfumo wa utoaji elimu ili kuleta manufaa kwa jamii inayotuzunguka.

Uhuru wangu wa kwanza nitaupata kwa kutodai nyongeza ya mshahara tena kwenye maisha yangu na sitolalamika tena kwamba mshahara ni kidogo kama nilivyokuwa nafanya huko nyuma bali ninakwenda kutumia kiasi hiki kidogo kutengeneza utajiri huku nikifahamu siku yeyote kiasi hiki pia kinaweza kisiwepo na hata nikifukuzwa kazi leo nitaendelea kufundisha mpaka mwisho wa maisha yangu ya hapa duniani.

Kinyagakelvin162@gmail.com
Blog;
https://kinyagakelvin.blogsport.com

0763766944.

No comments:

Post a Comment