Friday, 22 May 2020

Songombingo za bajeti........



Hongera sana kwa kuweza tupia jicho lako kwenye ukurasa huu, wapo wengi wangetamani kupata nafasi hiyo lakini hawakuweza, kwa Maradhi,kwasababu muda wao wakuwa duniani umepita na Kila namna nyingine kadha wa kadha,hivyo bahati hiyo usiitumie kusoma na kufurahia nenda kayafanyie kazi.

Leo tuangalie bajeti na changamoto zake, serikali yoyote huwa na kipindi ambacho kupitia bunge lake wanakaa na kupanga bajeti, hii inatupa picha kwamba bajeti ni kitu muhimu sana. Pamoja na umuhimu huo bado utakubaliana na Mimi bajeti ina changamoto zake, changamoto ya kwanza ni wakati gani mzuri wa kupanga bajeti?

Kosa kubwa ambalo wengi tunalifanya ni kupanga bajeti baada ya kuwa tumeshapokea fedha.

Tarehe 18/05/20 nilisoma makala bora sana kutoka kwa kocha ikieleza ni kipi cha kuanza nacho kati ya haraka na muhimu? Je nikikuuliza wewe kama unapaswa kuweka kipaombele kati ya haraka na muhimu utachaguwa kipi?

Sasa Mara nyingi tunapopanga bajeti baada ya kuwa tumeshapokea fedha huwa hatuweki uzito kwenye muhimu na tunaweka uzito kwenye haraka na pale muhimu vinapokuwa vimefikia muda wake huwa haviwezi kusubiri na hapo ndio wengi tunaingia kwenye mtego wa mikopo na madeni.

Nini cha kufanya?
Panga bajeti yako kabla hujapokea fedha unazotarajia au kipato chako, hapa utaona ni vipi muhimu unapaswa kuviwekea bajeti na achana na vingine vyote ambavyo utaviona vinahitaji haraka wakati umepokea fedha, maana wengi hawatumii bajeti kwenye maisha yao na wanaopanga bajeti pindi wakipata fedha wanatumia kwa vitu vingine vya haraka na vile muhimu vinawarudisha kwenye madeni.

Je matumizi muhimu ni yapi?
Hela ya chakula ni muhimu, ada za watoto,kodi ya nyumba, bili za Umeme, Maji,fedha ya dharula,fedha kwa ajili ya matibabu, lakini utakuta wengi kwasababu vitu hivi havihitaji fedha yako kwa Mara moja wengi wanajisaulisha na kusubiria mpaka muda utakapofika ndio waaenze kupambana nayo, lakini utakuta mavazi, michango ya sherehe ni vitu ambavyo wepesi kutoa, rafiki kanuni itakayokufanya ufanikiwe haijawahi kubadilika TUMIA KIASI KIDOGO KULIKO UNACHOPATA na hili litawezekana kupitia bajeti na ukishaweka bajeti yako kataa vishawishi vyovyote vile vitakavyojitokeza na kukulazimisha utumie nje ya bajeti yako.

Rafiki hiyo ni sehemu ndogo sana lakini ilishanitesa sana huko nyuma na kwasababu sipendi ukosee kama Mimi ndio ujifunze,  nakuletea makala hii ufanyie kazi ili tuvuke pamoja na kufurahia Zawadi ya maisha ambayo mungu katupatia bure kabisa, asante sana na nikutakie siku njema.

Mwl.Kelvin Kinyaga;
https://kinyagakelvin.blogspot.com
Email yangu
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944.

No comments:

Post a Comment