Thursday, 28 May 2020
"Wengi wape" kanuni iliyokuferisha bila wewe kufahamu....
Umepitia changamoto nyingi sana huko nyuma na nyingi umeshazisahau, amini hata hizi zinazokupa hofu sasa zitapita,usiogope pambana nazo na utakuwa salama,nakusalimu kwa jina la baba na naomba tuwe sote....
Rafiki Leo tuangalie kauli hii maarufu ya "WENGI WAPE" hii inatuambia kwamba maamuzi ya wengi huwa ni sahihi na kile wanachoamuwa wengi basi huwa hakipaswi kupingwa, ukiangalia kwa haraka haraka unakubaliana na usemi huu, na umeishi ukiamini hili na ndio maana umekutana na changamoto nyingi sana.
Kwanza nataka utambuwe kwamba hakuna hata mtu mmoja hapa duniani ambaye mnafafanana naye kwa Kila kitu hata kama ni pacha wako wa kufanana kabisa lazima kuna maeneo mnatofautiana, lakini jamii inataka tufanane, itakufananisha na wengine, kwa kukuambia usifanye hivi kwasababu haiwezekani, alifanya fulani na fulani na walishindwa, hii inatupa picha kwamba wengi tunaishi kwa kutumia vipimo vya wengine.
Nimeona hata makazini kuna maamuzi mengi yanafanywa na wengi wanakuwa na mtazamo fulani wa pamoja na mambo yanafuatwa kwa kutokana na wingi wao lakini baadaye Kila mtu anashangaa maamuzi haya yalipitaje mbona ni ya hovyo? Ni kwa kanuni ya wengi wape.
Sasa Leo tuangalie kwenye fedha Msemo huo kwanini umetuangusha sana.kutoka kitabu cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA mwandishi ameuliza swali moja linasema hivi;KWANINI ELIMU YA DARASANI NI KIKWAZO KWENYE FEDHA? ameeleza sababu kama saba hivi, lakini Mimi nakwenda kujadili na wewe sababu tatu, ukitaka kuzijuwa sababu zote nunua kitabu ukisome mwenyewe kina mambo mengi ambayo hatutaweza kuyachambuwa yote. Zifuatazo ni sababu tatu kwenye swali hilo hapo juu.
1.Mategemeo na msukumo kutoka kwenye jamii.
Jamii zetu zina mtazamo kwamba mwajiriwa ana kipato cha uhakika na kama mko ndugu wawili mmoja ni mwajiriwa na mwingine ni mfanyabiashara basi jamii itamtegemea zaidi mwajiriwa kuliko mfanyabiashara mdogo, wakati Mara nyingi huyu mfanyabiashara ana kipato kikubwa kuliko mwajiriwa,na hili huwa linaanzia kwenye familia, utegemezi kwa waajiriwa ni mkubwa zaidi na kwasababu mwajiriwa hajawahi Fanya biashara basi atakubaliana nao na kubeba majukumu yote bila hata ya kulalamika kumbe ndugu yake anatumia nafasi hiyo kujinyanyua.
2.Maisha ya maigizo
Kati ya kitu kinachotuangusha waajiriwa na wasomi ni kujiweka kwenye hadhi fulani ambazo siyo asilia, wengi watakuambia kwa degree yako utaanzishaje biashara ya genge? Ya kuuza vitafunwa, biashara ya juice?ndio maana utakuta wasomi wengi Kila siku wanazunguka na bahasha kutafuta ajira lakini kuna kazi nyingi za kuwaingizia kipato hawataki kufanya.Kama umeajiliwa basi uko tayari kuigiza maisha ambayo siyo viwango vyako ili kuwaridhisha wengine, utapandaje daladala si ukope ununue gari? Basi unasema mbona Kila mtu ananishauri hili unafanya.
3.Ujuaji mwingi na kutokuwa tayari kujifunza.
Wasomi huwa tunajidanganya kwamba tumeshasoma na tunajuwa Kila kitu na hivyo hatuko tayari kujishusha na kujifunza, pengine unakuta kijana katoka chuo kikuu, kafika ofisini kawakuta wenye uzoefu zaidi yao na ukizingatia elimu zetu ni nadharia zaidi, akifika ofisini kwakuwa waliopo wana elimu ndogo hataki kujishusha, nenda kampe wazo la biashara ndogo ndogo ya kumuingizia kipato utamuona atakavyokushangaa, kwa kudhani elimu walizo nazo zinawatosha ndio maana Kila siku wanaishi maisha ya kulalamika, ila kwa kujifunza Kila siku na kuchukuwa hatua bilashaka tungekuwa na jamii bora sana.
Rafiki yangu mtazamo wa wengi wape utakuchelewesha sana, jiulize swali ni kwanini 20% pekee ya watu duniani ndio matajiri na 80% wana maisha ya mahangaiko na ufukara? Kama ingekuwa wengi wape kwanini wasingekuwa wamefanikiwa 80% na 20% ndio masikini na vipato vya kati? Njia ya kwenda peponi ni nyembamba na ngumu ila ya kwenda kwenye moto wa Jehanamu ni pana na isiyo na vipingamizi, hivyo amua Leo wapi unataka kupita? Asante sana.
Bonyeza hapa chini
https://kinyagakelvin.blogspot.com
Kupata mafunzo yaliyopita zaidi ya 25.
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment