Monday, 25 May 2020

Kwanini wewe siyo tajiri?.......



Habari za wakati huu rafiki, kuweza kukutana na maandishi haya kunaonyesha kwamba u buheri wa afya na kwa hilo sote kwa pamoja tunayosababu kumshukuru mungu wetu.

Rafiki yangu ulishawahi fikiria siku moja Mtoto wako atakapopata ujasiri akakuuliza KWANINI WEWE BABA/MAMA SIYO TAJIRI? utamjibu nini? Ulishawahi fikiria swali hilo?

Basi kwenye kitabu cha RICH DAD,POOR DAD zipo hadithi kadhaa zinazoonyesha namna watoto wanavyoweza kutuuliza maswali hayo na kwenye kitabu hicho ipo siku moja  Robert alimuuliza baba yake kwanini wewe siyo tajiri?ndipo baba yake akampa jibu la kwamba yeye siyo tajiri kwasababu alichaguwa kuwa mwalimu na walimu hawapendi kuwa matajiri wanapenda kufundisha na hivyo kama anataka kuwa tajiri amuulize baba wa rafiki yake Mike atamfundisha kwani ana mipango mizuri ya kifedha. Hapa kwenye kisa hiki mwandishi anataka kutufundisha kwamba waajiriwa wengi hatupendi kujifunza kuwa matajiri na hivyo tunaridhika na kazi zetu,malipo ya mwisho wa mwezi yasiyotosha na kurudi tena kufanya kazi na kulipa madeni yetu,lakini kama tukitaka kupata elimu ya fedha darasani kwenye mfumo wa elimu masomo hayo hayafundishwi.

Adithi ya pili inatuelezea kisa ambacho mama mmoja anaadithia kuhusu Mtoto wake ambaye siku moja alikuja kutoka shule na kumuuliza swali hili;

"Why should I put time into studying subjects I will never use in real life?"
Akimaanisha kwamba ni kwanini aweke muda wake kwenye masomo,kujifunza mambo ambayo hatakuja kuyatumia kwenye maisha yake?

Ndio mama yake bila kufikiri akamjibu kwa kujiamini kwamba;
"If you don't get good grades, you won't get into college and if you don't graduate from college, you won't get a good job,And if you don't have a good job,how do you plan to get rich?
Akiwa na maana kwamba, kama hatopata maksi za juu hatoweza kwenda chuo na asipomaliza chuo hatopata kazi nzuri, sasa bila kazi nzuri atawezaje kuwa tajiri?

Hizi ndizo ngonjera zilizozoeleka huko mitaani kwetu lakini baada ya mama huyo kujibu hivyo ndipo Mtoto wake anamjibu kwa swali? JE MATAJIRI WOTE TUNAOWAFAHAMU WAMEPATA UTAJIRI KWASABABU YA ELIMU ZAO?

Hapo mama akawa mpole na kujisemea kwamba ni kweli tumekuwa tukijibu majibu tuliyozoea na kuambiwa na Wazazi wetu na hayo tunawaamishia watoto wetu wakati yameshapitwa na wakati.

Bilashaka lipo ulilo ondoka nalo rafiki yangu, nikutakie siku njema na wakati mzuri wa kutafakari maisha yako. Asante

Kinyagakelvin162@gmail.com
Blog yangu;
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944

No comments:

Post a Comment