Wednesday, 20 May 2020

Dhana mbili unazopaswa kuzijuwa kuhusu fedha....



Asubuhi huwa na nguvu pale unapoamka na kumshukuru mungu kwa uhai,kwa watu wazuri wanaokuzunguka,familia yako,mume au mke wako, watato kama umejariwa na vile vyote vinavyokupa nguvu ya kusonga mbele, lakini kuianza siku yako kwa kukumbuka watesi, adui zako au wale wote wanaokuchukia ni kuamua kukaa mbali na furaha na kuishi maisha ya chukizo.

Rafiki Leo tutaangalia dhana mbili zilizobakia kati ya tatu ambazo unapaswa kuzifahamu, kutoka kwenye kitabu cha Dr Makirita Aman cha ELIMU YA MSINGI KUHUSU FEDHA nilieleza dhana moja ambayo ni FEDHA,ukirejea makala yangu ya tarehe 09/05/2020 nilieleza kwamba fedha ni zao la Thamani, na haya makalatasi tunayoamini ndio fedha ni njia tu ya kubadilishana thamani, Leo tuangalie dhana mbili zilizobakia kuhusu fedha unazopaswa kuzifahamu.

1.Utajiri ni nini?
Yapo maneno mengi kwenye fedha tunayatumia bila kufahamu maana yake ni nini? Ukisikia neno tajiri bilashaka unafikiri mtu mwenye magari ya kifahari, nyumba nzuri na aina ya umiliki wa vitu vingi vya thamani, hebu tuone maana halisi ya neno Tajiri. UTAJIRI ni hali ya kuwa na kiasi cha kutosha,kupitiliza hata uhitaji ambao mtu anao. Hivyo basi unaweza kuwa na Utajiri kwenye eneo fulani lakini sehemu ambayo bado una uhitaji bado hujawa na utajiri, hivyo nyumba,magari na ufahari mwingine ni sehemu ndogo ya utajiri na ndio maana watu wengi wanapambana kupata utajiri na wakiupata wanagundua bado kuna vingi wanahitaji na kama furaha wanaweka hapo basi siku zote wanakuwa wamejinyima furaha.

2.Uhuru wa kifedha ni nini?
Unaweza kuwa na fedha na ukawa na utajiri lakini usiwe huru kifedha,hebu tuone maana halisi ya UHURU WA FEDHA ni pale ambapo mtu anakuwa hana tena hofu kuhusu fedha.mtu kwenye hatua hii ana uhakika wa kuendelea kuishi atakavyo mladi havunji sheria na maadili, hata kama hafanyi kazi moja kwa moja, hapa mtu anakuwa amefanya uwekezaji ambao hahitaji tena kulazimika kufanya kazi moja kwa moja ndio fedha iingie.

Kwa kufahamu dhana hizi tatu kifedha utakuwa umejuwa uko wapi kwenye uelewa kwenye fedha mpaka sasa na utajisukuma mpaka siku moja ufikie Uhuru kifedha. Basi tuangalie maswali matatu ambayo nimewahi kukutana nayo pale nilipojaribu kuelezea dhana hizi tatu za fedha.

A.Umesema fedha ni mbadilishano wa thamani je wanaocheza bahati nasibu na kushinda fedha nyingi wanakuwa wametoa thamani gani?
Hapa rafiki tunaweza kuona swali hili zuri linasibitisha kwamba kweli fedha ni mbadilishano wa thamani, hebu angalia watu hawa baada ya miaka kadhaa wanarudi kwenye maisha yao ya ufukala,tena unaweza kuta ni wa kutupwa Mara dufu, unawakumbuka washindi wa BSS?wengi wako wapi? Unafikiri ni kwamba hawakuwa na vipaji? Kama umepata fedha nyingi tofauti na thamani uliyotoa basi muda si mrefu utarudi ulikotoka.

2.Umesema utajiri ni kuwa na kiasi cha kutosha na kupitiliza hata uhitaji ambao mtu anao, je inawezekanaje mtu akafikia hatua akakosa uhitaji? Hapa ndio maana dhana hii huwa inawachanganya wengi, kwanza tufahamu mahitaji muhimu ni rahisi sana kuwa nayo ila gharama nyingi ni anasa za duniani, lakini kwanini tunapaswa kuutafuta utajiri bila kukoma? Wapo wengi sana wenye uhitaji, masikini, waremavu na wengine wengi wanaweza nufaika na utajiri, tunaangaika na vingi kwa ajili ya wengine na si kwa ajili yetu pekee, Doctor hakusomea udaktari ili aje kujitibu bali kutibu wengine.

3.Hiyo dhana ya Uhuru kifedha mbona ni ngumu, inawezekanaje mtu apate fedha bila ya kufanya kazi? Kwenye kitabu hiki ukikipata na kukisoma kimeeleza kwa kina kuna watu wanamiliki hisa nyingi kwenye makampuni, kuna mtu niliwahi msoma anamiliki nyumba za kupangisha zaidi ya 10000 je huyu anakuwa ameshafikia hatua kwamba alishafanya kazi huko nyuma lakini sasa fedha inamfanyia kazi yeye. Hii ni hali ambayo ukiifikia unakuwa na utosherevu mkubwa sana.

Rafiki siku zote pigana ukijuwa ni wapi unataka kufika na baada ya kuzifahamu dhana hizi tatu Nina imani akili yako imefunguka sana, kwa maswali zaidi kuhusu dhana hizi tatu tuwasiliane kupitia.

https://kinyagakelvin.blogspot.com
Email yangu; Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944.

No comments:

Post a Comment