Friday, 22 May 2020
Tatizo halipo kwa anayekulipa na kiasi unachopokea.......
Hongera rafiki kwa siku hii ya Jumamosi ya tarehe 23/05/2020 hakuna siku nyingine itakayo kuja ikafanana na siku kama hii kwa Kila kitu, lakini bado sisi binadamu tulio wengi tunazichukulia siku kama vile ni kitu ambacho tunacho muda wote na milele, basi kwa Mimi rafiki yako kukumbusha hilo sitegemei kama unakwenda kuipoteza siku ya Leo kwa kufanya yale uliyozoea kufanya.
Rafiki yangu Jana niliandika makala yenye kichwa cha habari kinachosomeka SONGOMBINGO ZA BAJETI,kwenye makala ile nilieleza changamoto baadhi ambazo wengi tunakutana nazo na kujikuta tunaingia kwenye madeni, na kwa kunukuu makala kutoka kwa kocha toka kwenye kitabu cha THE WAR OF ART na kusema kutofahamu nini cha kuanza nacho kati ya HARAKA na MUHIMU na kuorodhesha matumizi muhimu ni yapi baadhi ya rafiki zangu walionyesha kutoridhika na Maelezo yale kwa msingi wa maswali mawili ambayo nitayatolea ufafanuzi hapa chini.
1.Unafanyaje pale matumizi muhimu yanapokuwa makubwa kuliko kipato chako?
Baada ya kumnukuu mwanafalsafa Seneca kwamba matumizi muhimu ni machache ila anasa ndio gharama na nyingi yupo mmoja hakukubaliana na hilo kwa kusema Je kusomesha, kujenga nyumba,chakula, mavazi hayo ni Anasa? Nilimuomba awe mtulivu na Leo nakwenda kumjibu.
Rafiki kitu ambacho kinawagharimu wengi ni kuishi maisha ambayo hawalingani nayo, naweza ita maisha ya Jirani zao, utakuta mtu anapoelezea matatizo ya kifedha aliyo nayo na madeni aliyo nayo kwasababu ya matumizi muhimu aliyonayo unaweza kumuonea huruma na kukubaliana naye, tatizo ni kwamba wengi tunaangalia tulipoangukia na siyo tulipojikwaa, kosa ambalo wengi tunalifanya ni kuyapa mambo umuhimu kwa kufuata mkumbo, mfano wengi wanaingia kwenye madeni kwa kisingizio cha kulipia wototo ada, lakini swali ni je kipato chako kinaruhusu wewe kupeleka watoto wako kwenye shule unazowapeleka? Au kwasababu umeona watoto wa Jirani wanasoma shule nzuri na wewe hutaki kuonekana wa chini unawapeleka? Hivi ndivyo tunavyoendesha maisha yetu kwenye Kila kitu,lazima mwanzo ukubali kuishi chini ya kipato chako na kisha ufanye jitiada za kukiongeza bila ya kukaa na kusubiria mwajiri wako, Fanya biashara na jishughulishe.
2.Swali la pili nililoulizwa ni JE UNAVYOSISITIZA MARA NYINGI NA KUTUONYESHA MADENI NI KITU KIBAYA MBONA KUNA WENGI WANAFANIKIWA KUPITIA MIKOPO?
Nadhani swali hili kwa wanakisima cha maarifa wanaelewa vizuri na huko mbele tunavyoendelea kuchambuwa vitabu utajifunza kwa kina kupitia kitabu cha elimu ya msingi kuhusu fedha, lakini kwa Leo nikupe siri moja ambayo unapaswa kuijua unapokopa, kabla hujakopa jiulize maswali mawili NANI ATALIPA? na swali la pili NITATOA WAPI? unakuta mtu anakopa kwasababu kipato hakitoshi na wakati huo huo atapaswa kulipa kupitia kipato hicho hicho, Kwanini wengine wanakopa na kufanikiwa? Jibu ni kwasababu wanakopa wao lakini hawalipi wao, mfano mfanyabiashara anaweza kukopa kwasababu tayari anawateja lakini hana mtaji, hivyo anapokopa anafahamu mteja wake ndiye atakayelipa deni hilo, Je kivipi? Pengine nimekopa milioni mbili ili niongeze mtaji kwenye biashara yangu,milioni mbili ikazalisha milioni tatu, hata kama natakiwa nilipe liba laki tano bado nitabaki na faida ya laki tano. Hivyo hiyo ziada yote imetokana na wateja wake lakini siyo kwenye kipato chake cha awali.
Rafiki yangu tuendelee kuwa pamoja Nina hakika tutavuka pamoja, tamaa yangu ni kuiona Tanzania yetu inaondokana na ufukara huu kupitia mafanikio ya mtu mmoja mmoja, hivyo tambuwa hakuna aliyezaliwa kwa ajili yako hivyo kumlaumu boss wako au serikali ni kuchaguwa kushindwa.
Mwl.Kelvin Kinyaga
https://kinyagakelvin.blogspot.com
Email yangu ni;
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment