Sunday, 17 May 2020
Kama wewe mwenyewe umeshajiambia huwezi kupata basi hakuna atakayekupatia.........
Rafiki yangu habari za wakati huu, Nina imani hujambo na unafurahia maisha pamoja na yale yote unayopitia, karibu tushirikishane machache ili tuwe na msingi imara kwenye maisha yetu....
Rafiki kwenye maisha yetu kuna vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wetu,vitu ambavyo tunaweza vikabili na kuvibadili vile tunavyotaka sisi, lakini vipo ambavyo hatuna uwezo wa kuvizuia au visiweze kutukuwepo au kuwepo, mfano hata kama hutaki mvua inyeshe huna uwezo wa kuizuia kutonyesha kwasababu huna uwezo nalo, habari njema ni kwamba kwenye fedha na utajiri ni wewe mwenyewe ndio unayejiwekea ukomo, na zipo kauli mbili ambazo zinatumiwa na watu ndio zinazoamua hatima zetu.
SIWEZI KUPATA/NITAPATAJE
Rafiki kama nilivyokushirikisha kutoka kwenye moja ya vitabu vinne ambavyo uchambuzi Wangu unaegemea zaidi ni kitabu cha RICH DAD,POOR DAD kwa utafiti aliofanya mwandishi unaonyesha kwamba masikini au watu wasio na kipato cha kutosheleza ni wepesi sana kutumia neno SIWEZI KUPATA,utasikia akisema siwezi kupata kiasi hicho kwani ni kikubwa sana, siwezi kuendesha gari,siwezi kuweka akiba, lakini watu waliofanikiwa hawatumii kauli hiyo kwani ni kauli inayoonyesha kukata tamaa na kutoushughulisha ubongo kufikiri, lakini wao hutumia kauli ya NITAPATAJE watu wengi walioshindwa neno nitapataje hulitumia pale wanapotaka matumizi ya anasa kwa fedha ambazo hawana, pengine hapo ndio hutumia neno nitapataje? Na kwa haraka ukimbilia kukopa na pindi akipata fedha hulipa deni na kukopa tena, lakini kama unataka kufanikiwa usijiambie SIWEZI KUPATA UTAJIRI Bali anza kufikiri NITAPATAJE UTAJIRI? hapo unaifanya akili ianze kufikiri kwa mapana na kuwaza ni nini ifanye kukupatia unachotaka, rafiki unaweza kuona hizi ni kauli ndogo zisizo na maana lakini nikuambie tu kwamba jikague kwenye kauli hizi na badilika Mara moja kwani huwezi fikia mafanikio ya juu kwa kuwa mwepesi kusema siwezi kwa mambo yanayowezekana.
Makala hii imeandikwa na Mwl.Kelvin Kinyaga
https://kinyagakelvin.blogspot.com
0763766944
Kinyagakelvin162@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment