Monday, 18 May 2020

Bidii ya kazi pekee haitoshi kukupa uhuru wa kifedha......



Rafiki yangu hongera kwa majukumu na hatua unazochukuwa Kila siku kwani bila kupiga hatua au kuchukuwa maamuzi yoyote tofauti na mazoea na kutarajia mabadiliko ni kujidanganya, kwani huwezi Fanya kitu kile kile ulichozoea kufanya na kwa namna ile ile na kukaa usubirie mabadiliko, huko ni kujidanganya,ni Sawa na kwenda chini ya muembe na kutarajia kuokota maparachichi, Kila siku jiulize LEO NIMEFANYA NINI CHA ZIADA TOFAUTI NA JANA?.........

Rafiki Leo tuangalie dhana ya FANYA KAZI KWA BIDII, kama siku zote ninavyosema mafanikio yoyote hupatikana kwa muunganiko wa vitu vingi, bidii kwenye kile unachofanya peke yake haitoshi kukupatia mafanikio.

Hebu tuangalie adithi kutoka kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN THE BABYLON,hapa tunakutana na marafiki wawili Bansier na Kobbi,Kobbi anamkuta Bansier amekaa akitafakari kwa kina,anamuomba amuazime Shekeli mbili na Bansier anamjibu kama angekuwa na hizo shekeli mbili basi asingethubutu kumpa yeyote kwani na yeye anaziitaji, Basi Kobbi anamuambia Bansier kama hana fedha kwanini asiendelee na kazi ya kutengeneza magari yaliyopo ili apate fedha? (Bansier alikuwa fundi magari) na hapa Bansier anamjibu Kobbi kwamba alishafanya sana kazi na kupata hela nyingi huko nyuma lakini mwisho wa siku anajikuta hana kitu na amerudi kwenye maisha ya awali na kwa Hili Kobbi anakubaliana na Bansier kwani amekuwa akifanya kazi kwa bidii na anapata fedha lakini baada ya muda anarudi kule kule, baada ya kufikiri kwa kina wanakumbuka yupo tajiri mmoja mkubwa sana anaitwa Arkad ni bora waende wakamuulize ni wapi wanakosea ili waweze kurekebisha.

Hapa tunajifunza somo kubwa sana kwamba unaweza ukaweka bidii kwenye kazi na ukapata fedha lakini kwasababu huna elimu ya fedha hujuwi fedha inatakiwa iwekezwe wapi ili ikufanyie kazi, kwani kama Kila siku unaifanyia kazi je ni kwa vipi unatakiwa uiwekeze ukiipata ili ikufanyie kazi na usirudi kwenye hatua za mwanzo, Je ni wangapi wanaendesha maduka yao kwa zaidi ya miaka 20 na yapo vile vile hayakui? Wangapi wameweka bidii kwenye kazi na bado hawajapata kile wanachotaka?

Basi rafiki yangu tuendelee kuwa pamoja kwenye chambuzi za vitabu hivi yapo mengi ya kukufumbuwa macho, asante na siku njema.

https://kinyagakelvin.blogspot.com
Kinyagakelvin162@gmail.com
0763766944
#Tuvuke pamoja


No comments:

Post a Comment